VIGEZO NA MASHARTI

Utangulizi

Vigezo hivi na masharti vinaongoza matumizi yako ya tovuti hii; kwa kutumia tovuti hii, unakubali vigezo na masharti haya kwa ukamilifu. Kama hukubaliani na vigezo na masharti haya au sehemu yoyote ya vigezo na masharti, usitumie website hii.

Unapaswa uwe na si chini ya miaka 18 ili kuweza kutumia tovuti hii.Kwa kutumia tovuti hii. Kwa kutumia tovuti hii na kwa kukubaliana na vigezo na masharti, unathibitisha kwamba una umri wa miaka si chini ya 18.

Tovuti hii inatumia kuki. Kwa kutumia tovuti hii na kwa kukubaliana na vigezo na masharti haya, unakipa idhini chama chetu ya kutumia kuki kwa mujibu wa vigezo vya sera ya faragha/kuki ya ACT Wazalendo.

 

Ruhusa ya kutumia tovuti

Isipokuwa mahala itakavyotajwa vingine, ACT Wazalendo na/au watoa ruhusa wake wanamiliki haki zote za hatimiliki kwenye tovuti na vitu vilivyomo kwenye tovuti. Kulingana na ruhusa ya hapo chini, hatimiliki zote zimehifadhiwa.

Unaweza kuangalia, kupakua na kuchapisha kurasa na maudhui mengine kwa matumizi yako binafsi tu, kulingana na ukomo uliowekwa hapo chini na kwengineko kwenye vigezo na masharti.

Hauruhusiwi:

  • kuchapisha upya vitu kutoka kwenye tovuti hii (ikiwemo kuchapisha upya kwenye tovuti nyengine);

  • kuuza au kukodisha vitu kutoka kwenye tovuti hii;

  • kuonesha vitu vya kwenye tovuti kwa umma;

  • kuzalisha upya, kurudia, kunakili au kutumia vitu kutoka kwenye website hii kwa malengo ya kibiashara;

  • kuhariri au kubadilisha vitu vilivyomo kwenye tovuti; au

  • kusambaza vitu kutoka kwenye tovuti hii isipokuwa maudhui maalumu yaliyotolewa kwa ajili ya kusambazwa.

Ambapo maudhui yamewekwa kwa ajili ya kusambazwa, yatalazimika kusambazwa katika shirika lako tu.

 

Matumizi yanayokubalika

Haupaswi kutumia tovuti hii katika njia yoyote ile amabayo inasababisha, au inaweza kusababisha, hasara kwa tovuti au kuharibu upatikanaji au ufikiwaji wa tovuti; au katika njia yoyote ambayo ni kinyume na sheria, utapeli au lengo baya au shughuli.

Haupaswi kutumia tovuti hii kunakili, kuweka, kutuma, kutumia, kuchapisha au kusambaza kitu chochote ambacho kinajumuisha (au kinahusiana na) kirusi chochote cha kompyuta.

Haupaswi kufanya aina yoyote ya ukusanyaji wa taarifa (kama vile kuchimba taarifa) kwenye tovuti hii bila ya kupata idhini ya maandishi kutoka ACT-Wazalendo.

Haupaswi kutumia tovuti hii kusambaza au kutuma matangazo ya kibiashara ambayo hayakutafutwa.

Haupaswi kutumia tovuti hii kwa lengo lolote linalohusiana na masuala ya masoko bila kupata idhini ya maandishi kutoka ACT-Wazalendo.

 

Ukomo wa upatikanaji

Upatikanaji waa baadhi ya maeneo kwenye tovuti hii umewekewa ukomo. ACT-Wazalendo ina haki zote za kuweka ukomo wa ufikiwaji wa baadhi ya maeneo kwenye tovuti hii, au kwenye tovuti hii yote, kadiri ACT Wazalendo itakavyoamua.

Kama ACT Wazalendo itakupatia utambulisho na neno siri kukuwezesha kufikia maeneo yaliyozuiliwa katika tovuti hii au maudhui mengine au huduma, unapaswa kuhakikisha kuwa utambulisho na neno lako la siri vinabaki kuwa siri yako tu.

ACT Wazalendo inaweza kusitisha utambulisho wako na neno siri lako kama inavyoweza kuamua bila ya taarifa au maelezo yoyote.

 

Maudhui ya mtumiaji

Katika vigezo na masharti haya, “maudhui ya mtumiaji yako” yanamaanisha vitu (bila ya kutoa maandishi, picha, sauti, video) ambazo unaweka kwenye tovuti hii, kwa malengo yoyote yale.

Unaipatia ACT Wazalendo leseni ya kidunia, isiyobatilishika ya kutumia, kuzalisha, kuanzisha, kuchapisha, kutafsiri na kusambaza maudhui yako katika chombo cha habari kilichopo au cha baadae. Pia unaipatia ACT Wazalendo haki kutoa leseni ya haki hizi na haki ya kuchukua hatua dhidi ya uvunjwaji wa haki hizi.

Maudhui ya mtumiaji wako hayapaswi kuwa haramu au kinyume na sheria na yasitowe uwezekano wa kupelekea wewe au ACT Wazalendo ichukuliwe hatua za kisheria au sehemu ya tatu (katika kesi yoyote chini ya sheria yoyote).

Haupaswi kuwasilisha maudhui yoyote kwenye website ambayo ambayo yameshawahi kukabiliwa na hatua za kisheria au malalamiko yanayofanana na hayo.

ACT Wazalendo ina haki ya kuhariri au kutoa kitu chochote kilichowasilishwa kwenye tovuti hii, au kilichopo kwenye ‘servers’ za ACT Wazalendo, au kilichochapishwa kwenye website.

Licha ya kwamba ACT Wazalendo ina haki chini ya vigezo hivi na masharti kwa maudhui ya watumiaji, ACT Wazalendo haiangalii uwasilishwaji wa maudhui hayo, au uchapishwaji wa maudhui hayo, kwenye tovuti hii.

 

Hakuna waranti

Tovuti hii inatolewa “kama ni” bila ya uwasilishaji au waranti kuhusiana na tovuti hii na vitu vinavyowekwa kwenye tovuti hii.

Bila ya kuathiri mantiki ya paragraph ifuatayo, ACT Wazalendo haihakikishi kwamba:

  • tovuti hii itapatikana muda wote, au kupatikana kabisa; au

  • taarifa kwenye tovuti hii ni kamilifu, za kweli, sahihi, na zisizopotosha.

Hakuna chochote kwenye tovuti hii kinachosemwa kuwa, kukusudiwa kuwa, ushauri wa aina yoyote. Kama unahitaji ushauri kuhusu suala lolote la kisheria utapaswa kutafuta mtaalamu anayehusika.

 

Ukomo wa uwajibikaji

ACT Wazalendo haitawajibika kwako (iwe chini ya law of contact, the law of torts au vinginevyo) kuhusiana na maudhui ya, au matumizi ya, au vinginevyo kuhusiana na tovuti hii:

  • kwa website kutolewa bila malipo, kwa upotevu wowote ule;
  • kwa upotevu wowote maalumu au wa moja kwa moja;
  • kwa upotevu wowote wa kibiashara, upotevu wa mapato, kipato, faida au akiba iliyotegemewa, upotevu wa mikataba au uhusiano wa kibiashara, upotevu wa heshimaa, au upotevu au uharibifu wa taarifa.

Ukomo huu wa uwajibikaji utafanya kazi hata kama ACT Wazalendo imeshauriwa juu ya hasara inayoweza kupatikana.

 

Umaalumu (Exceptions)

Hakuna chochote kwenye angalizo la tovuti hii litakalozouia au kuweka ukomo wa dhamana inayotolewa na sheria kwamba itakuwa ni kinyume na sheria kuzuia au kuweka ukomo; na hakuna chochote kwenye angalizo la tovuti hii litazuia au kuweka ukomo uwajibikaji wa ACT Wazalendo kuhusiana na:-

  • utapeli au uwakilishaji usio sahihi wa utapeli; au

  • jambo ambalo litakuwa ni haramu au kinyume na sheria kwa ACT Wazalendo kuzuia au kuweka ukomo, uwajibikaji wake.

 

Mantiki

Kwa kutumia tovuti hii, unakubali kwamba utolewaji na uwekwaji wa ukomo wa uwajibikaji ni wa wa mantiki, yaani yanaingia akilini.

Kama unadhani hayana mantiki yoyote, haupaswi kutumia hii website.

 

Wahusika wengine

Unakubali kwamba, kama taasisi inayojiendesha kwa kuandikisha wanachama wapya, ACT Wazalendo ina maslahi katika kuweka ukomo uwajibikaji binafsi kwa watumishi wake na waajiriwa. Unakubali kwamba hutaleta dai lolote binafsi dhidi ya watumishi na waajiriwa wa ACT Wazalendo kuhusiana na upotevu wowote utakaoupata kuhusiana na tovuti hii.

Bila ya kuathiri aya inayofuata, unakubali kwamba uwekwaji wa ukomo kwenye dhamana na uwajibikaji uliowekwa bayana kwenye angalizo la tovuti hii utawalinda watumishi, waajiriwa, mawakala, wakandarasi wa ACT Wazalendo na ACT Wazalendo yenyewe.

 

Vifungu visivyotekelezeka

Kama kifungu chochote cha angalizo la tovuti hii hakitekelezeki chini ya sheria inayotumiwa, au kitaonekana hakitekelezeki, hiyo haitaathiri utekelezaji wa vifungu husika vya angalizo la tovuti hii.

 

Fidia

Unakubali kuikomboa ACT Wazalendo na kuhakikisha unailinda ACT Wazalendo dhidi ya upotevu, uharibifu, hasara na gharama (ikiwemo bila kuwepo kwa ukomo wa gharama za kisheria na kiwango chochote kinacholipwa na ACT Wazalendo kwa mtu wa tatu katika utatuzi wa madai au mzozo kwa kuzingatia ushauri wa wanasheria wa ACT Wazalendo) iliyopatwa na ACT Wazalendo inayotokana na ukiukwaji unaofanywa na wewe wa kifungu chochote cha vigezo na masharti haya [au inayotokana na dai lolote kwamba umekiuka kifungu chochote cha vigezo na masharti haya].

 

Ukiukwaji wa vigezo na masharti haya

Bila kuathiri haki nyengine za ACT Wazalendo chini ya vigezo na masharti haya, ukikiuka vigezo na masharti

haya kwa namna yoyote ile, ACT Wazalendo inaweza kukichukulia hatua kitendo hicho kadiri itakavyoona inafaa kukabiliana na ukiukwaji huo, ikiwemo kusitisha upatikanaji wa tovuti kwako, kukupiga marufuku usije kwenye tovuti, kuzuia kompyuta inayotumia anuani yako ya IP isiingie kwenye tovuti, kuwasiliana na mtoaji wako wa huduma ya intaneti kuwaomba wazuie usiingie kwenye tovuti na/au kukufungulia kesi Mahakamani.

 

Tofauti

ACT Wazalendo inaweza kuvidarisi vigezo na masharti haya mara kwa mara. Vigezo na masharti yaliodarisiwa yataendelea kufanya kazi kwa ajili ya tovuti hii kuanzia siku ya ya uchapishwaji wa vigezo na masharti yaliodarisiwa kwenye tovuti hii. Tafadhali pitia ukurasa huu mara kwa mara kuhakikisha kwamba unauzoefu na vigezo na masharti ya sasa.

 

Zoezi/kazi

ACT Wazalendo inaweza kusafirisha, kutoa kandarasi au kushughulika na haki na/au wajibu wa ACT Wazalendo chini ya vigezo na masharti haya bila kukujulisha au kupata ridhaa yako.

Huwezi kusafirisha, kutoa kandarasi au kudhughulika na haki na/au wajibu wako chini ya vigezo hivi na masharti haya.

 

SERA YA FARAGHA

Taarifa zinazokusanywa

ACT – Wazalendo (“Chama”) kinakusanya taarifa zitakazo kiwezesha kukutambua wewe binafsi, kama vile jina lako, anuani yako, nakadhalika (“taarifa binafsi”) pale tu zitakapo tolewa kwa hiari kwetu na wewe au na mtu wa tatu (kama vile wakala wa usafiri) kwa niaba yako. Tunakusanya taarifa binafsi zinapotolewa kupitia fomu zetu kwenye tovuti zetu, app za simu za mkononi, kwenye maongezi ya simu, kupitia barua au barua pepe au kwa kuonana uso kwa uso.

Tovuti hii haikusanyi au kuhifadhi taarifa yoyote binafsi kutoka kwako wakati wa kutembelea tu tovuti hii, labda kwa hiari yako au kwa makusudi utupe hizo taarifa (kwa mfano, baada ya kufanya maombi ya mtandaoni au kwa kuomba taarifa zaidi).

Seva zetu hukusanya wenyewe baadhi ya taarifa za kiufundi, zisizokuwa za binafsi wakati unapotumia tovuti hii au app za simu za mkononi (“taarifa zinazoweza kutumika”). Taarifa za kiufundi zinaweza kujumuisha aina ya kivinjari (browser) unachotumia, mfumo wa operesheni (operating system), muda ukurasa umeangaliwa (page views), taarifa za mahala (location data), anuani ya IP (IP address) nakadhalika.

 

Utumikaji wa taarifa

Tunatumia taarifa zako binafsi kutimiza lengo ambalo taarifa hizo zimetolewa kwalo, au vinginevyo liliwekwa na sera hizo. Kwa mfano, tunaweza kutumia taarifa zako binafsi kama kwa ajili ya:

✔  kufanyia kazi ombi lako la kuwa mwanachama na malipo;

✔  kukusajili kwenye kanzidata ya Uanachama na taratibu za kujitolea;

✔  kukutafuta kuhusiana na masuala ya uanachama;

✔  kufanyia kazi maombi yako ya kubadilisha uanachama wako au akaunti yako ya matumizi;

✔  kukupatia uzoefu unaoendana na wewe kwenye tovuti yetu;

✔  kujibu maswali yako na aina zingine za mawasiliano;

✔  kukusajili ili uweze kupokea barua pepe zetu kuhusu kampeni au taarifa zingine ambazo umeonesha kuvutiwa nazo; na

kukidhi matakwa ya kisheria.

 

Unaweza kuamua kutopokea barua pepe zozote kuhusu kampeni muda wowote kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja au kwa kufuata viunganishi vya “jitoe” au “unsubscribe” kwenye hizo barua pepe utakazokuwa unaletwa. Tunaweza, hata hivyo, kuendelea kukutafuta tukiwa na habari tunazodhani zinaendana na wewe, hususani kulingana na maombi yako ya zamani au yanayokuja.

Tunaweza kutumia taarifa zinazotumika tunazokusanya kwa sababu yoyote tunayoona inafaa, ikiwemo kuboresha, kutunza, au kuendesha tovuti zetu na huduma zetu.

 

Usambazaji wa taarifa

Hatutouza taarifa zako binafsi kwa yoyote nje ya chama chetu. Tutazionesha taarifa zako binafsi kwa mtu wa tatu pale tu kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo na muhimu kufanya matumizi yanayokubalika yaliyoelezwa katika sehemu ya “MATUMIZI YA TAARIFA” ya sera hii. Kwa mfano, tunaweza kusambaza taarifa zako kwa:

✔  watu wanaoshughulika na malipo yetu, wakandarasi wanaohusika na msaada wa kiufundi na wateja wetu, na watoa huduma wetu ambao wanahitajika kuziweka taarifa binafsi katika mazingira ya siri na wanaozuiwa kuzitumia kinyume na huduma wanazotoa kwa niaba yetu; na

✔  mamlaka za kiserikali na kisheria au mtu mwengine yoyote wa tatu kwa kiwango ambacho inahitajika kutii matakwa ya kisheria.

 

Usalama wa taarifa binafsi

Chama kinakuhakikishia usalama wa taarifa zako binafsi. Tunatumia njia za uhakika wa kibiashara na kiufundi katika kulinda taarifa zako binafsi zilizo katika hifadhi yetu, na tovuti yetu inatumia soketi salama ya kukusaidia kulinda faragha yako ya taarifa za kadi ya malipo, jina, anuani, barua pepe na taarifa nyengine nyeti unazotupatia.

 

Kuki na wasifu

Chama na wenza wetu katika masoko waanaweza kutumia kuki, pikseli zisizoonekana kupata taarifa kuhusiana na wageni wa tovuti zetu na app za simu za mkononi. Kuki maandishi madogo ambayo huwekwa kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi ambacho aambayo wakati unatembelea tovuti au unatumia app ya simu. Tunatumia kuki kwenye tovuti na app zetu ili kuzifanya taarifa unazopatiwa ziendane na wewe, kuhifadhi taarifa kama vile tarehe, nakadhalika, kukuruhusu kuingia kwenye tovuti kwa urahisi, na kufuatilia mwitiko wa matangazo yetu.

Unaweza kuipangilia kumpyuta yako ili ikujulishe kila wakati kuki inatumwa au kuzima kuki zote (isipokuwa flash kuki) kupitia kwenye kivinjari chako. Angalia sehemu ya Msaada kwenye kivinjari chako au mipangilio iliyokuja na simu yako ya mkononi kuangalia jinsi ya kufanya hivyo. Baadhi ya vifaa vya mkononi huhifadhi kuki si kwenye maeneo yaliyoounganishwa kwenye kivinjari tu bali pia ambayo ni maalumu kwa app fulani, ambayo hayawezi kudhibitiwa na mipangilio ya kivinjaro. Angalia mipangilio ya chaguzi za app kwenye kifaa chako cha mkononi na ujifunze jinsi ya kudhibiti au kufuta kuki ambazo zinaweza kuwa zimewekwa kwenye maeneo mengine. Kama hutaki kuki, baadhi ya vipengele, huduma au shughuli ambazo zinapatikana kwenye tovuti zetu au app za mkononi vitaathirika sana na unaweza usiwe na uwezo wa kufanya baadhi ya shughuli au kufikia baadhi ya maudhui. Uamuzi wa kukubali au kukataa kuki ni tofauti na uamuzi wako wa kukubali/kukataa jumbe za barua pepe.

Pia tunatoa matangazo kupitia teknoljia ya matangazo ya mtu wa tatu. Katika hatua ya kukuletea matangazo ya wahusika wetu wa tatu kwako, kuki ng’ang’anizi za kipekee zinaweza kuwekwa kwenye kompyuta yako au kifaa cha mkononi kusaidia kuthibiti matangazo yetu ya mtandao, kutambua wakati gani kifaa fulani kimetembelea tovuti yetu, kufahamu matangazo gani huwaleta watu kwenye tovuti zetu, na kuweka kumbukumbu kama kuna ombi limetolewa. Taarifa ambazo sisi na watoaji wetu wa matangazo

tunakusanya kupitia teknolojia haiwezi kutambuliwa kibinafsi lakini hutumika kutengeneza wasifu usio na jina ambao humruhusu mtoaji wa matangazo kutoa matangazo yaliyolengwa kwako na unavyovipenda katika mtandao mzima wa utoaji wa matangazo.

Tovuti zetu kwa sasa haziwezi kupokea amri ya “Usinifuatilie” ambazo zinaweza kutumwa na kifaa chako au kivinjari.

 

Viunganishi kwa tovuti za wahusika wa tatu

Tafadhali fahamu kwamba tovuti za wahusika wa tatu zinazopatikana kupitia viunganishi vilivyopo kwenye tovuti yetu kila moja ina sera yake ya faragha na utaratibu wa ukusanyaji taarifa. Watuna udhibiti, wajibu au dhamana kwa tovuti hizi za wahusika wa tatu au sera zao na maudhui yao. Hatuwezi kuhakikishia usalama wa taarifa yoyote unayoiweka wazi kwa wahusika wa tatu.

 

Mabadiliko kwenye sera hii

Tunaweza kuiboresha sera hii kulingana na wakati na mahitaji. Tutakuwa tunaischapisha sera ya zamani kwenye tovuti na tutaonesha juu kabisa ya sera lini sera mpya ilipitishwa. Tafadhali pitia sera hii mara kwa mara ili upate kufahamu maboresho mapya kwenye utaratibu wetu wa faragha.

 

Ukali

Kama kifungu cha vigezo na masharti haya kitagundulika na mahakama yoyote au mamlaka bobezi kuwa kinakiuka sheria na/au hakitekelezeki, vipengele vingine vitaendelea kufanya kazi. Kama kifungu chochote kinachokiuka sheria na/au hakitekezeki kitaendana na sheria na kutekelezeka kama sehemu ya kifungu hicho itafutwa, kipengele hicho kitaonekana kimefutwa, na sehemu iliyobakia ya kifungu hicho kitaendelea kufanya kazi.

 

Makubaliano yote

Vigezo hivi na masharti haya yanajumuisha makubaliano yote kati yako na ACT Wazalendo kuhusiana na utumiaji wako wa tovuti hii na yanatengua makubaliano yote ya awali kuhusiana na matumizi yako ya tovuti hii.

 

Sheria na mamlaka

Vigezo hivi na masharti haya yataongozwa na, na kufahamika, kulingana na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) Kanuni, 2020, na mzozo wowote unaohusiana na vigezo na masharti haya utakuwa chini ya mamlaka za mahakama za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK