Kuhusu ACT

Chama cha ACT Wazalendo kilianzishwa mnamo mwaka 2014 na ni chama kinachoendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania. Sisi ni vuguvugu lenye lengo la kutengeneza Tanzania huru, yenye maendeleo na mafanikio ambayo misingi yake itakuwa ni uhuru, uwajibikaji, na uwazi.

Dira yetu ni kwa Tanzania kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kupitia:

  1. Kujenga uchumi shirikishi unaoshamiri na wenye kukua na kuweza kutengeneza ajira.
  2. Miundombinu imara inayochochea sekta zote za uchumi unaokuwa.
  3. Upatikanaji wa elimu bora.
  4. Upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  5. Kujenga taasisi ya polisi huru na inayozingatia taaluma ili iweze kuwahudumia na kuwalinda watu wote.
  6. Muungano wenye kuweka maslahi ya watu wa pande zote mbele, wa haki na wa usawa utakaowekewa msingi wake kwenye Katiba ya watu.
  7. Vita dhidi ya rushwa na aina zote za ufisadi.
  8. Utoaji wa hifadhi ya jamii iliyobora kwa wasiojiweza, masikini na watu wengine wasiojiweza.
  9. Makazi ambayo watu wanaweza kuyamudu, na kupatikana kwa wote.
  10. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa watu wote.

alt

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK