Ukiwa mbunge wa zaidi ya kipindi kimoja unaweza kupima tofauti ya maendeleo ya wananchi kwa kiashiria cha matatizo ya wananchi unayoyapokea kwa kuyasikiliza. 

Bunge la 10 wananchi wengi wa Kigoma waliokuja kuniona nyumbani au ofisini ( Mimi husikiliza wananchi wote wa majimbo yote ya Kigoma bila kubagua) walikuwa na malalamiko ya kiuzalishaji ( ama kutozwa kodi au ushuru mkubwa, kukosa pembejeo za kilimo za ruzuku ama kuomba fursa za kazi kwenye miradi mbali mbali ya umma au sekta binafsi).

Sasa hivi Hali ni tofauti Kabisa. Wananchi wana changamoto ambazo ni za kuishi ( survival). Kwa waliosoma Maslow hierarchy of needs Hii ni ile ya kwanza kabisa ya mahitaji ya msingi. Wengi wanasema biashara zimekufa na mitaji imekata. 

Wengine kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mdogo riba za mikopo waliyochukua kwenye taasisi za fedha zimepandiana na mali zao kuuzwa.

Ndani ya kipindi kifupi nimeshuhudia watu ninaowajua wakiporomoka kurudi kwenye dimbwi la umasikini. Serikali inapaswa kufanya survey ya hali ya wananchi na kuja na mkakati wa kuwaokoa vingivevyo hali itakuwa mbaya sana