Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo) tarehe 25 Machi 2017 kitafanya Mkutano Mkuu Maalum wa Kidemokrasia wa kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha, Mkutano husika utajadili miaka 25 ya Utekelezwaji wa Azimio la Arusha nchini Tanzania na miaka 25 ya kutelekezwa kwa Azimio husika.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kutoa mada kwenye mkutano husika ni ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo, Mama Anna Mghwira, Mwenyekiti wa Taifa ACT Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, Mshauri wa Chama ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Mawasiliano ya Umma ACT Wazalendo pamoja na viongozi wengine mbalimbali.

Wageni waalikwa ni pamoja na Dkt. Bashiru Ally, Mhadhiri Mjamaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ndugu Njelu Kasaka, Mtumishi wa Umma na Mwanasiasa Mkongwe, shuhuda wa miaka 50 ya Azimio la Arusha pamoja na Katrin Voss, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa chama cha kijamaa cha Ujerumani – Die Linke.

Mahali: Corridor Springs Hotel
Mkoa: Arusha
Siku: Machi 25, 2017
Muda: Saa 4 asubuhi – 12 jioni
 

Event Date: 
March 25, 2017
Venue: 
Corridor Springs Hotel