Leo kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kigoma ( RCC ) kinakutana chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Hili ni Kama Bunge la Mkoa na inakutanisha Wabunge wote wa mkoa, Mameya na Wenyeviti wote wa Mammlaka za Serikali za Mitaa, Wakuu wa Wilaya wote mkoani na Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Kwa mbunge yeyote makini hivi sio vikao vya kukosa kwani ndipo mnapata nafasi ya kuunganisha mawazo yote ya mkoa na kuyapigania bungeni.

Pamoja na ajenda za Bajeti, Leo tuna ajenda ya kuendeleza Zao la Mchikichi ambapo mkoa unataka kupanda michikichi 15m na kuanzisha viwanda saba vya kusindika mazao ya mawese