Lengo na ndoto kuu ya Chama chaa ACT-Wazalendo ni kujenga Taifa lenye kujitegemea kiuchumi na kiutamaduni, na ambalo linalinda na kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, na uongozi bora. Katika kufikia lengo la kulinda na kudumisha ustawi wa jamii, Hifadhi ya jamii ni nyenzo muhimu mno kwetu ACT Wazalendo.

Hifadhi ya jamii ni mfumo imara na endelevu wa kuwajengea uwezo na utayari wananchi katika kukabiliana na matatizo ya majanga ya kiuchumi na kijamii.Hifadhi ya jamii husaidia sana kutoa usalama na uhakika wa kiuchumi, kijamii na kiafya. Hii ni njia ambayo serikali, mwajiri na mwajiriwa huchangia kiasi fulani cha mapato yake ya sasa kwa ajili ya kumsaidia baadaye atakapokuwa hana uwezo wa kupata kipato cha uhakika.

Aidha, hifadhi ya jamii husaidia wafanyakazi katika sekta ya umma  na binafsi kukabiliana na gharama za matibabu na matatizo mengine ya kijamii. Tafiti zinaonyesha kuwa uwezo wa hifadhi ya jamii kwa watu wengi iwezekanavyo katika nchi huchangia kupunguza hali ya umasikini na hivyo kuipandisha nchi kiuchumi na kijamii. Hifadhi ya jamii pia huchochea uwekaji wa akiba katika nchi na hivyo kuwezesha uwekezaji wa ndani na kupanua shughuli za uzalishaji mali. Hata hivyo, ni wananchi wachache sana walioopo katika mfumo rasmi wa hifadhi ya jamii (kwa takwimu za mwaka 2015 ilikuwa ni 6% tu ya watanzania wote).

Chama cha ACT-Wazalendo kinaamini kwamba wananchi wote wanapaswa kuwa katika mfumo rasmi wa hifadhi ya jamii, na kitaendelea kupigania kuhakikisha hili linatokea kabla au baada ya kuunda serikali.