Afya
Tanzania ni nchi kubwa na yenye idadi kubwa zaidi ya watu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuwa uchumi umekuwa ukikua kwa takribani asilimia saba (7) kwa mwaka, ukuaji huu haujionyeshi katika kuboreka kwa hali ya maisha ya wananchi wa kawaida. Kwa mujibu wa Taarifa ya Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu kufikia asilimia 3 kwa mwaka na idadi ya watu ambao wanaishi katika umaskini wa kutupwa (ufukara) imeongezeka kwa idadi ya zaidi ya watu milioni moja.

Ongezeko hili la idadi ya watu maskini linamaanisha ongezeko la watu ambao hawana uhakika wa huduma bora za jamii. Maana yake ni kuwa tuna watanzania wengi wanaoshambulika zaidi na magonjwa yanayozuilika lakini wasiokuwa na uhakika wa kupata matibabu, tuna watanzania wengi wasio na maji safi na salama na tuna watanzania wengi wasiopata huduma ya elimu bora, nafuu nay a uhakika.

Tanzania ina mfumo dhaifu wa huduma za afya usiotoa fursa sawa za kinga na tiba kwa watu wote na hasa wenye kipato cha chini. Aidha, tafiti zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watoa huduma hawana weledi wa kutosha na hawawajibishwi ipasavyo katika kutoa huduma kwa wananchi. Falsafa inayoongoza sera ya chama cha ACT Wazalendo juu ya sekta ya afya ni kuwekeza katika kuboresha taaluma na uwajibikaji katika sekta ya afya, na kuwekeza katika huduma za kinga na kutoa fursa sawa kwa huduma za kitabibu ili kipato kisiwe kikwazo kupata huduma hizo.

ACT Wazalendo pia inaamini kwamba elimu ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi. Kiwango chetu cha elimu kwa maana ya idadi na ubora kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo bila kuzitatua mapema iwezekanavyo mchango wa sekta ya elimu katika maendeleo ya nchi hautaonekana. Tafiti zinaonyesha kuwa watoto na vijana wengi wanaopita katika mfumo wetu wa elimu hawapati maarifa na stadi stahiki na elimu yetu hawaiandaa kukabiliana na changamoto za Karne ya 21.

Kwa kuzingatia hali hii, Chama cha ACT-Wazalendo kitaendelea kuhimiza kuwekeza katika maeneo muhimu ya elimu yanayolenga kuinua viwango vya kujifunza kwa wanafunzi Ili kupanua fursa na kuboresha viwango vya ubora katika elimu katika ngazi zote. Kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa walimu ndio msingi mkuu wa kujifunza na kuboresha elimu, Chama chetu kitahimiza kuwekeza katika kuweka mfumo imara wa motisha na uwajibikaji kwa walimu.

Pamoja na hayo ni lengo pia la ACT Wazalendo kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, hasa wananchi wa vijijini ambao wengi wao sasa hawana